.br

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

.br ni ya ccTLD ya Brazil. .br ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1989 kwa kiwango cha pili cha majina. Jina hili lilisajiliwa na wajumbe wa kamati ya mawasiliano ya Brazil (Brazilian Internet Steering Committee ) mpaka mnamo mwaka 2005, ambapo kituo cha mawasiliano ya kimtandao Brazil (Brazilian Network Information Center) kiliposhika hatamu na hadhi ya kusajili jina hili.Kituo hiki kinaruhusu usajili wa majina hata kwa lugha ya kireno.[1]

.Ikumbukwe kwamba kabla ya nchi ya Brazil haijaunganishwa katika mtandao mpana wa mawasiliano ya intaneti mwaka 1991, matumizi ya .br yalikuwa mahsusi kwa taasisi za kitaaluma/kielimu tu. Mwaka 1995 chombo kiitwacho "Internet Management Committee of Brazil" kiliundwa kwa minajili ya kuratibu ugawaji wa majina na anwani za kimtandao kwa makampuni ya mawasiliano ili yawe mawakala wa kusambaza huduma hii kwa watu wengi zaidi nchini humo.

Reference[edit | edit source]