.ga

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

.ga ni kikoa cha nchi ya Gabon, kikoa hiki kimetokana na herufi mbili za mwanzo za Gabon. Kilianzishwa mwaka 1998 na kinaendelea kutumika mpaka leo! Taasisi yenye dhamana ya kusajiri vikoa katika nchi hii ya Gabon ni Gabon Telecom na ndiye mdhamini. Hii ni baada ya kuwa chini ya shirika la posta na simu la jamhuri ya Gabon mpaka mwaka 2013. Matumizi yanayotegemewa ni yale yote yenye uhusiano na Gabon wakati matumizi halisi ni kwa shirika lolote lilokubaliwa na nchi. Baadhi ya maingizo yanatumia muundo usio rasmi mfano:- amb-jina.ga kwa ubalozi ch-jina.ga au chu-name.ga kwa mahospitali ot-jina.ga kwa ofisi za utalii nk [1]

Marejeo[edit | edit source]