CGI.br

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

The Brazilian Internet Steering Committee (CGI.br) iliundwa kwa mstakabali 147 baina ya idara za serikali, mnamo Mei 31, 1995, ambao ulifanyiwa marekebisho kwa kauli ya rais 4,829 ya Septemba 3, 2003, kwa lengo la kupanga na kujumuisha miradi yote ya huduma za mtandao nchini Brazil, na pia kuboresha ufundi, ubunifu, and utoaji wa huduma zilizopo.
CGI.br inajumuisha wanachama kutoka serikalini, sekta ya mashirika, sekta zinginezo na jamii ya wasomi.
Kwa kuzingatia maadili ya wadau wengi, uwazi, na demokrasia, kutokea Julai 2004 CGI.br imekuwa ikiwachagua kidemokrasia wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kifaida kushiriki mijadala na mazungumzo na serikali kuhusu vipaumbele vya mtandao.

Wanachama wa CGI.br[edit | edit source]

CGI.br ina wanachama 21 kama ifuatavyo:

Wawakilishi 9 kutoka serikalini.

 • Wizara ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu
 • Wizara ya Mawasiliano
 • Waziri kutoka afisi ya rais
 • Wizara ya Ulinzi
 • Wizara ya Maendeleo, Viwanda, na biashara ya nchi za kigeni
 • Wizara ya Upangaji, na Bajeti
 • Idara ya Taifa ya habari
 • Kamati ya Taifa ya Sayansi na Maendeleo ya Teknolojia
 • Kamati ya Taifa ya ukatibu ya Sayansi, Teknohama na maswala ya habari -CONSECTI

Wawakilishi 4 kutoka sekta ya mashirika

 • Watoa huduma za mtandao
 • Watoa huduma za mawasiliano
 • Sekta ya maunzi na program
 • Biashara zinazotumia mtandao

Wawakilishi 4 kutoka sekta ya tatu

Wawakilishi 3 kutoka jamii ya Sayansi na Teknolojia

Gwiji mmoja wa mtandao

References[edit | edit source]

CGI.br