Jackie Treiber

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

Jackie Treiber ni mkurugenzi mtendaji mweza wa ICANNWiki[1]. Amekuwa katika nafasi hii tokea Februari, 2015. Makao yake ya kazi na makazi ni Portland, Oregon.

Mbali na kazi yake ya ICANNWiki, Treiber huudhuria IGF[2], ambako amezungumza kwenye paneli zinazohusiana na kuboresha maudhui ya lugha mbalimbali kwenye mtandao (2016) pamoja na uzoefu wa kujitegemea wa jinsia na upatikanaji wa mtandao (2017).

Treiber pia ni mwana sanaa na mwandishi.

Historia ya Kazi[edit | edit source]

ICANNWiki (2015+)[edit | edit source]

Akiwa kama mkurugenzi mtendaji mwenza wa ICANNWiki, Jackie hufanya kazi karibu na Dustin Phillips ambaye ni mbunifu wa michoro na mhariri, Vivian Hua pamoja na mkurugenzi wa tovuti, Raymond King kutengeneza na kuhariri maudhui ya tovuti. Jackie pia huudhuria mikutano yote ya ICANN ili kudumisha na kuimarisha uhusiano na wanachama wa ICANN na kuchangia michango kwenye tovuti ya ICANNWiki kupitia matukio ya kufikia kama vile ICANNWiki Edit-a-thon and ICANNWiki Ambassador Program.

Flashgiovani (2012)[edit | edit source]

Flashgiovani ni mradi maalum wa manispaa ya Bologna, Italia. Kama mwandishi huko Flashgiovani, Treiber ilifanya mambo ya ubunifu na maarifa yanayohusiana na maisha huko Portland, Oregon. Pia alitafsiri makala za Kiitaliano kwende kwenye Kiingereza kwa manufaa ya wanaozungumza lugha ya Kiingereza.

The Portland Review (2010-2011)[edit | edit source]

The Portland Review imechapisha mashairi, vitu vya kusadikika na uhakiki wa umuhimu tokea mwaka 1956. Kama mhariri mkuu wa the Portland Review, Treiber aliomba kazi kutoka kwa waandishi na wanasanaa wanaoanza mara tatu kwa mwaka. Pia alianzisha matukio ya ufikiaji kama vile masomo ya uandishi na vidokezo vidogo vidogo vya waandishi wa kuchagua.

Elimu[edit | edit source]

Jackie alipokea stashahada ya sanaa kutoka chuo kikuu cha jimbo la Portland mnamo mwaka 2014, ambapo alijizatiti katika fasihi na uandishi wa ubunifu

Marejeo[edit | edit source]

  1. ICANNWiki. Imepatikana 4 Oktoba 2017
  2. Internet Governance Forum. Imepatikana 3 Oktoba 2017.