Changes

Jump to: navigation, search

Portal:Internet Governance

1,728 bytes added, 3 years ago
no edit summary
Kongamano la '''WSIS''' la Tunis liliweka bayana swala la maana ya utawala wa mtandao, likaorodhesha maswala ya utawala wa mtandao, na kubuni kongamano la utawala wa mtandao {'''Internet Governance Forum (IGF)'''}, kitengo cha washika dau kilichoundwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa {UN Secretary General} – Koffi Annan.

'''WSIS+10'''

WSIS ilisherehekea miaka 10 tangu kongamano la Tunis (2005). Kwenye kongamano la Tunis, kulikuwepo na maelewano kuwa utawala wa mtandao (IG) udhihirishe uhalisia wa washika dau wote (multi-stakeholders).

Kuendelea ushirikiano ilikuwa mbinu ya aina yake iliyolenga uundaji wa mstakabali mpya wa wahishika dau wote (multi-stakeholders) katika utawala.

Miaka 10 tangu matukio ya WSIS, washika dau husika (RIRs, mataifa, mashirika ya kijamii, wanasheria walijihusisha kwenye kuchunguza matokeo yake ndani ya muongo huo. Matokeo haya yaliwakilishwa kwenye kongamano la umoja wa mataifa (UNGA), jijini New York , Disemba 2015.

'''Internet Governance Forum (IGF)'''

Mojawapo wa matokeo ya kongamano la WSIS ilikuwa ni kuanzisha kongamano la kimataifa la utawala wa mtandao (IGF), ili kuwezesha washika dau kuchangia kwenye mazingira ambayo yataratibu uundaji wa sera za umma.

Kongamano la kwanza la IGF liliandaliwa Athens, Ugiriki (2006), kongamano la pili (Rio de Janeiro, Brazil-2007), kongamano la tatu (Hyderabad, India-2008), kongamano la nne (Sharm el Sheikh, Misri-2009), Kongamano la tano (Vilnius,Lithuania-2010), sita (Nairobi, Kenya-2011), saba (Baku, Azerbaija-2012), nane (Bali, Indonesia -2013), tisa (Istanbul, Uturuki -2014), kumi (Joao Pessoa, Brazil -2015).

Mwaka huu kongamalo la kumi na moja litaandaliwa mji wa Guadalajara, Mexico (Disemba).

'''MAG (Multi-stakeholder Advisory Group)'''

Ni jopo linalowajibika kuandaa kongamano la IGF kila mwaka.

Kando na kongamano kuu la IGF, kuna makongamano ya kitaifa (local IGF), kimaeneo (regional IGF) mfano East Africa IGF, West Africa IGF, Southern Africa IGF, na Africa IGF.

Navigation menu