PRISM

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

PRISM
Programu ya kisiri inayotumiwa na idara ya usalama ya Marekani NSA, kukusanya mawasiliano yanayofanyika kwenye mtandao. Mpango huu wa kisiri ulizinduliwa mnamo mwaka wa 2007 na serikali ya George W. Bush.

Bado mengi ayajulikani kuhusu jinsi programu ya PRISM inavyofanya kazi. Programu inaruhusu NSA kukusanya mawasiliano ya watu kutoka kampuni kubwa duniani za tekinolojia kama Google, Yahoo, Facebook, Microsoft, Apple, na wengine.
Mpango wa PRISM ulifichuliwa mwaka 2013 na Edward Snowden ambaye alikuwa mkandarasi wa NSA.
Hali hii ya kufichua siri ya mradi huu wa PRISM ilimlazimu Snowden kutoroka nchini Marekani na kuomba hifadhi nchi ya Urusi baada ya utawala wa Obama kutangaza nia yake ya kumkamata na kumfungulia mashtaka kwa kigezo cha kufichua siri.

Marejeo[edit | edit source]

theverge. Retrieved 19 September 2017