TCP/IP

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

Transmission Control Protocol/Internet Protocol[edit | edit source]

TCP/IP ni kiwango chenye umuhimu mkubwa sana kwenye mtandao.
Viwango vya TCP/IP vinawekwa na shirika la Internet Engineering Task Force IETF. Kutokana na umuhimu wake, TCP/IP ni mojawapo wa kiwango kinachopewa umakinifu wa hali ya juu kwenye mtandao na shirika la IETF.

Jinsi TCP/IP inavyofanya kazi[1]

Ili vifaa viwili viweze kutumiana ujumbe kwa njia hii ya TCP/IP, kwanza lazima vifaa viwe vimeungwa katika mtandao (inteneti) na pia ni lazima vifaa vyote viwe huru.

kifaa kinachohitaji kutuma ujumbe/data lazima kwanza kitume taarifa ya kuomba njia ili kifaa cha pili kiweze kurusu au kukataa.Upande wa pili wa mawasiliano utarudisha ishara ya kuonyesha kama nafasi ipo au hakuna iwapo bado kuna mawasiliano na sehemu nyingine. iwapo nafasi haipo ishara itarudishwa kwenye chanzo kuonyesha kuwa mawasiliano hayawezi kufanyika katika vifaa hivyo. Hii ni sawa na mawasiliano katika simu, iwapo watu wawili wanawasiliana kwa njia ya simu na mtu mwingine akajaribu kupiga simu katika mmoja wapo, kwa hiyo simu haitaweza kupokelewa kuunganishwa hadi wamalize maongezi yao.

Iwapo vifaa vya mtandao vitakuwa huru baada ya kupeana ishara, vitaunganishwa moja kwa moja ili viweze kutuma ujumbe/data bila kuingiliwa na mawasiliano kutoka sehemu nyingine.

Reference[edit | edit source]