Twitter

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

Twitter ni mtandao wa kijamii unaowezesha watumiaji kutuma na kusoma jumbe fupi zenye nukta 140 – zinazoitwa “tweets”.
Watumiaji waliojisajili wanaweza kusoma na kutuma “tweets”, ilhali wale ambao hawajajisajili wanaweza kusoma tu.
Watumiaje wanaweza kuingia Twitter kupitia mtandao, kitumizi cha ujumbe mfupi (SMS) au simu ya rununu.
Makao makuu ya Twitter Inc. ni San Francisco, California, Marekani na ina zaidi matawi au afisi 25 kote duniani.
Twitter ilibuniwa mnamo Machi 2006 na Jack Dorsey, Evan Williams, Biz Stone, na Noah Glass, na ikazindukiwa Julai 2006.
Kufikia Machi 2016, Twitter inajivunia zaidi ya watumiaji milioni 310 wanaotuma karibia tweets milioni 340 kwa siku.