TzNIC

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

TzNIC au Tanzania Network Information Center ni shirika lililoanzishwa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) ikiwa na jukumu la kusimamia na kudhibiti operesheni za ccTLD kwa Tanzania, .tz. Ikiwa pia na jukumu la kusimamia kikoa ngazi ya pili chini ya .tz. TzNIC ilianzishwa tarehe 16 ya November 2006 kwa cheti cha ujumuisaji chenye nambari 58303. Kituo kilianzishwa kama kampuni ndogo kwa mujibu wa sheria ya Tanzania (kurasa ya 212)

HISTORIA[edit | edit source]

Mnamo mwezi Juni 1993, waTanzania watatu, Prof. Beda Mutagahwa, Bill Sangiwa na Kitalima Mabula, kwa msaada wa Randy Bush, walianzisha mkakati wa kusajili na kuanzisha .tz ccTLD. Kwa mujibu wa viwango vya ISO-3166, ccTLD ilisajiliwa na IANA na ICANN. Usajili ulifanikiwa kwa msaada wa serikali ya muungano wa Tanzania, kazi ya kuhakikisha maendeleo ya Internet nchini ilianzishwa na Prof. Beda akiwa kama mkurugenzi wa University Computing Center na Randy Bush akiwa kama mtu wa mawasiliano ya kiufundi kwa ajili ya ccTLD. .tz ilianza kazi mwezi Agasti 1994. 2005 kati kati, ilianzishwa kamati kutawaza TzNIC kuwa na opareta wa ccTLD. Mnamo Aprili 30 2010, ICANN iliidhinisha uhalali wa .tz kwa TzNIC.

KAZI ZA TzNIC[edit | edit source]

kazi muhimu zinazofanywa na TzNIC ni kama zifuatavyo:

  • Utaratibu na usimamizi sahihi wa kikoa .tz
  • Kufikia kiango cha kimataifa cha usimamizi wa ccTLD kikoa ngazi ya pili yanayohusiana.
  • Kusajili kikoa chenye muongozo sahihi kwa watumiaji, na kufanya kazi inayohusisha wasajili na usajili kwa kanuni sahihi na usimamizi wa usajili wa kikoa.
  • kutoa muongozo mara kwa mara kuhusu usimamizi na usajili wa kikoa .tz.
  • kutoa taarifa na kujenga ufahamu juu ya utaratibu mbalimbali na mahitaji muhimu kwa ajili ya usajili wa kikoa
  • kutoa matangazo muhimu kuhusu mabadiliko kwa miongozo,sera au kanuni zinazohusiana na usajili wa kikoa .tz

FAIDA KUU ZA TzNIC[edit | edit source]

  • kukupa utamburisho kirahisi ukiwa mtandaoni
  • Uaminifu
  • urahisi wa kutatua migogoro ya kimtandao ndani ya nchi

MUUNDO[edit | edit source]

Wanachama wa TzNIC ndio wapo juu ya kufanya sehemu kuu ya mfumo shirika, ikifuatiwa na Kamati ya sera na ushauri (PAC) halafu msimamizi. msimamizi huratibu afisa sheria, afisa wa kifedha na afisa ufundi na ofisi ya katibu msimamizi. Mhasibu msaidizi humsaidia afisa wa kifedha na mhandisi wa mfumo humsaidia afisa ufundi

marejesho[edit | edit source]

tznic.com.[1]
  1. tznic.com,About tzNIC.