Zantel

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

Zanzibar Telecommunication (Zantel) ni kampuni ya mawasiliano yenye makao makuu jijini Dar es salaam, likini ikiwa imejikita zaidi  katika kutoa huduma huko Zanzibar (Tanzania visiwani), ilianzishwa mnamo mwaka 1999.  Zantel ina idadi ya wafanyakazi kuanzia 201 hadi 500 hivyo kusaidia pia katika kupunguza tatizo la ajira nchini Tanzania.[1]

Kampuni ya zantel inajihusisha na utoaji wa huduma za mawasiliano kama upigaji wa simu, ujumbe mfupi wa maandishi pamoja na huduma za data kwa njia ya  CDMAS, GSM na 3G. Kampuni ya Zantel ilizindua huduma zake za 3G mnamo mwezi wa tano mwaka 2012, lakini mpaka hivi sasa Zantel inatoa huduma za 4G katika baadhi ya mikoa ukiachilimbali huduma za 3G na 2G ilizokuwa ikizitoa .

Hata hivyo Zantel inatoa huduma za  mfumo wa wireles na ya kutumialaini za waya kwa watumiaji  zaidi ya 3,070,000 na 10,147 tangu mwezi Machi mwaka 2013. Zantel ina 11.2% ya soko la hisa  katika wireless na hisa 6.0% katika soko la laini za waya tangu mwezi machi mwaka 2013.

Zanteli pia imefanikiwa kuanzisha huduma za kibenki kupitia huduma yao ya” Ezypesa” ambayo ni rahisi na ninafuu pia kuitumia.

Pamoja na hayo kampuni ya zantel imefanikiwa kuingia ubia na kampuni za:-

1.Emirates Telecommunications Corp  yenye asilimia ya hisa 65

2.Serikali ya zanzibar yenye jumla ya hisa asilimia 18% na

3. Meeco International Tanzania  yenye jumla ya hisa asilimia  17.[1]

References[edit | edit source]

  1. Zantel. Retrieved 28 Apr 2017.