Domain Names

Kutoka Swahili ICANNWiki
Pitio kulingana na tarehe 20:26, 15 Julai 2018 na Henry Mwinuka (Majadiliano | michango) (MAELEZO KUHUSU ANUANI ZA KIMTANDAO)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Rukia: urambazaji, tafuta

JINA LA KIKOA Katika maendeleo ya Teknolojia na habari, moja ya vitu ambavyo ni vya msingi kuvitambua na kuvizingatia ni namna ambavyo watumiaji na wafaidika wa teknolojia ya intaneti wanavyoweza kutumia mtandao wakiwa katika mazingira tofauti tofauti. Ikumbukwe kuwa ili mtu aweze kutumia mtandao basi anapaswa kuwa na anuani namba na anunai jina ambavyo ndivyo vitamtambulisha na kumuunganisha katika mfumo wa kimawasiliano wa mtandao. Kama vile ambavyo katika maisha yetu ya kila siku tunaishi kwenye makazi yenye anuani ili kuweza kutambulika kwa urahisi, vivyo hivyo tunapaswa kuwa na anuani zinazotutambulisha huko mtandaoni. Anuani hiyo hujulikana katika lugha ya kiswahili kama jina la kikoa.

Anuani hizi au jina la Kikoa kama ilivyoandikwa hapo awali, zipo katika aina mbili yaani zile ambazo husimamiwa moja kwa moja na shirika lisilo la faida la masuala ya anuani za kimtandao au anuani tovuti pamoja na jina au majina ya kikoa ambalo makao yake yako Nchini Marekani. Mfano wa majina ya kikoa ambayo huratibiwa na Shirika hili ni yale yanayoishia na .com,.org, .net, .eu, .un na kadhalika.

Lakini pia zipo anuani za kimtandao ambazo huwa zinasimamiwa na mamlaka za nchi mbalimbali. Anuani hizi huhusisha zaidi watumiaji walio ndani ya mipaka ya nchi fulani. Baadhi ya Nchi kama Tanzania imepitisha kanuni ambazo zinalazimisha watumiaji wote wa mtandao kujisajili kwa kupitia mamlaka iliyopo ndani ya Nchi ambacho kinajulikana kama Kituto Cha Uunganishaji Mifumo ya Kimtandao Tanzania. Hivyo basi majina yote ya vikoa Nchini Tanzania huishia na neno .tz.
REJEA 1. https://www.icann.org/resources/pages/tlds-2012-02-25-en 2. https://tznic.or.tz/index.php/en/ 3. https://cyber.harvard.edu/property00/domain/main.html