IANA

Kutoka Swahili ICANNWiki
Pitio kulingana na tarehe 07:16, 4 Septemba 2017 na Aziz Zeenath (Majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Rukia: urambazaji, tafuta

Internet Assigned Numbers Authority (IANA) ni idara ya ICANN yenye jukumu la kudumisha usajili wa kitambulisho cha kipekee cha internet inayojumuisha domain names, vigezo vya itifaki na namba za mtandaob([IP Addresses] na [Autonomous System Numbers]).

IANA inasambaza vitalu vya [IP] addresses kwa Regional Internet Registries ([RIRS]) tano (5)

Maelezo ya jumla[hariri | hariri chanzo]

Kadiri internet inavokuwa, kulikuwa na haja ya kitengo kitacho shughulikia yafuatano:

  • Kuchukua jukumu la usimamizi
  • Kuhakikisha kila mtu anatumia itifaki na mihimili yenye kufanana
  • Kuratibu kazi za watambulishaji
  • kuhakikisha uumbaji na mgao wa anwani na majina ya kikoa yanafanyika ipasavyo, kufuatia misingi ya sheria inayokubalika na kila mtu.

Shirika lililopewa majukumu kwa mahitaji haya ni IANA. Kutokana na ukuwaji wa internet mnamo miaka ya 1990 pia ilihitajika shirika ambalo litakuwa na jukumu ya usajili wa majina ya kikoa na anwani. Hivi ndio ICANN (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers) ilipoanzia.

[[ICANN] ina jukumu la kusajili shughuli zinazohusiana na IP numbers,kusajili na itifaki mbali mbali za DNS, lakini ICANN haichukui nafasi ya IANA. Kunatofauti nyingi kati ya ICANN na IANA, hasa kuhusiana na sifa, malengo na majukumu yao

IANA vs ICANN[hariri | hariri chanzo]

  • IANA ni taasisi inayoendesha TLDs (Top-Level Domains) na inahusika na kazi za IP addresses na safu zake, na sifa zingine zinazohusiana.
  • ICANN inahusiana na mkataba wa ufahamu ([[MoU]), ni taasisi inayoendesha IANA.

Kazi za IANA[hariri | hariri chanzo]

  • Pamoja na kusimamia DSN root zone, pia IANA inasimamia usajili wa .int na .arpa
  • Kuhusu rasilimali za namba, IANA ina haki ya kuratibu IP kimataifa kwa mtiririko wa nafasi ya nambari, na kuzigawa kwa RIR (Regional Internet Registries)
  • IANA inawakilisha hifadhi kuu ya usajili wa nambari na majina ya itifaki.

Majina ya Kikoa[hariri | hariri chanzo]

IANA ina jukumu la kutawala majina ya kikoa ambayo inahusosha mahusiano na waendeshaji wa TLD,na waendeshaji wa root name server, pamoja na kuendesha .int na .arpa.

Ili kuwezesha na kuboresha usimamizi na mgao wa Internationalized Domain Names (IDNs), IANA iliendeleza "IDN tables" inayosambaza taarifa zinazohusiana na kukubalika katika lugha mbalimbali na taarifa zinazohusiana na TLD.

Vigezo vya Itifaki[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na itifaki za IETF, IANA ina wajibu na kusimamia mpango wa URI (Uniform Resources Identifier) na character encoding kwa matumizi ya mtandao.

Anwani za IP[hariri | hariri chanzo]

Anwani ya IP ni kitambulisho cha pekee ambayo hupewa kwa kila kifaa ili kuunganishwa katika mtandao kama vile kompyuta, simu za mkononi, printer n.k.

IANA ina wajibu wa ujumbe wa anwani za IP kwa RIRs. Na kwa upande wao kila [RIR] (regional Internett Registry) ina wajibu wa kugawa anwani za IP kutegemea na eneo inayosimamia, IANA inatathmini maombi na huweza kuongeza mgao wa ziada kwa RIR.

Mkataba wa IANA[hariri | hariri chanzo]

Awali kazi za IANA zilikuwa zikisimamiwa na Information Science Institute (ISI) katika Chuo Kikuu cha California kusini kupitia uongozi wa Dr. Jon Postel chini ya mkataba wa Defense Advance Research Project Agency (DARPA).

Mwaka 1997, Serikali ya Marekani chini ya utawala wa Rais Bill Clinton, iliidhinisha kupitishwa kwa usimamizi wa kiufundi wa Domain Name System (DNS), ikiiwa pamoja na kazi za IANA kuwa sekta binafsi. Tarehe 30 Januari, 1998, Department of Commerce (DOC) ilitoa makala Green Paper ikipendekeza kuanzishwa kwa shirika jipya, binafsi yasiyo ya faida kupata usimamizi wa DNS. Wadau wa mtandao kimataifa walifikisha maoni na mapendekezo yao kuhusiana na Green Paper, ambayo yalikusanywa na kusomwa na NTIA. Mnamo Juni 1998, NTIA ilichapisha White Paper, iliyobeba taarifa ya sera ya serikali ya Marekani kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya uongozi wa kiufundi wa DNS kwa kutengenezashirika jipya kulingana na kanuni za utulivu, ushindani, uratibu binafsi chini-juu na uwakilishi.

November 25, 1998, Department of Commerce iliitambua rasmi ICANN kama shirika jipya lenye jukumu la kuongoza DNS kupitia mkataba wa ufahamu uliosainiwa na pande zote mbili. Hii ikiwa kama matokeo ya "DSN Wars"

Department of Commerce ilitoa mkataba kwa ICANN kusimamia kazi zote za IANA tarehe 9 Februari, 2000. Makubaliano haya yalichapishwa upya tena mwaka 2001, 2003 na 2006. Mkataba wa 2006 ulibadiliishwa mara kadhaa. Marekebisho ya hivi karibuni yaliongeza mkataba wa ICANN hadi 30 Septemba, 2012.

Kumalizika kwa muda wa mkataba kazi wa Internet Assigned Numbers Authority (IANA), awamu mpya ya ICANN ilianzishwa na National Telecommunication and Information Administration's (NTIA's) iliotangazwa Machi 2014.

Awamu hii (mabadiliko ya uendeshaji wa IANA) ilitarajiwa kukamilika mnamo tarehe 30 Septemba, 2015.

Taarifa ya uchunguzi wa DOC kwa kazi za IANA[hariri | hariri chanzo]

25 Februari,2011, DOC kupitia NTIA ilitoa Noti of Inquiry(NOI) kupitia mkataba wa kazi za IANA. Mkataba wa kazi za ICANN IANA ulikuwa hadi 11 September,2011. Interet community ilihimizwa kutoa maoni juu ya maswali mbalimbali yaliyochapishwa na NTIA kusaidia kubiresha kazi za IANA. NOI ilikuwa mapitio ya kwanza yaliyofanywa na DOC kwa kuwa ICANN ilichukuwa jukumu la IANA mwaka 2000. Mwisho wake ulikuwa 31 Machi,2011.

ICANN ilikubali umuhimu wa mapitio ya kina ya mkataba wa kazi za IANA. ICANN ilipendekezza mabadiliko ya hali ya mkataba wa ununuzi kati ya serikali ya Marekani na bodi uongozi wa mtandao kuwa na makubaliano ya ushirika. Kwa kuongezea ICANN pia ilipendekeza pamoja na kanuni za uwajibikaji na uwazi katika mfumo wa makubaliano unaofuatia na kuzuia upeo wa kazi za IANA. ICANN ilihitaji kuendeleza kazi iliyokuwepo ya IANA kwa kuingia mkata tofauti na Internet Architecture Board (IBA) na Internet Engineering Task Force (IETF) kufanya programu ya usajili wa vigezo na kazi za usimamizi wa .arpa top level domain name (TLD).

14 Juni, 2011, DOC ilitowa Further NOI kutafuta maoni ya umma kuhusu rasimu yake ya kazi (Statement of Work-SOW), ambayo ilikuwa na muhtasari wa maoni yaliyotolewa na umma juu ya NOI ya kwanza, majibu ya NTIA, na mahitaji ya kina ya kazi kwa kazi za IANA.

Mashirika 46 ndani ya jumuiya ya mtandao wa kimataifa waliwasilisha maoni na majibu yao kwa SOW.[[]]

=RFP kwa mkataba mpya wa kazi za IANA[hariri | hariri chanzo]

Kufuatia NOI, DOC ilichapicha Ombi la Mapendekezo (Request for Proposal-RFP) kwa ajili ya mkataba mpya wa kazi za IANA mnamo 10 Novemba,2011. Vyama vilivovutiwa vilihimizwa kuwasilisha mapendekezo yao hadi kufikia 12 December, 2011.Mkataba mpya ulipangwa kuanza kazi 1 April, 2012. hadi 31 Machi, 2015. Chama kilichokubali kubeba kazi za IANA kilipewa hiari ya kuongeza muda wa makubaliano kwa miaka mitatu mbele.

Baadhi ya wanachama wa