ICANN 101

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

ICANN[edit | edit source]

ICANN ni mshika dau mkuu ulimwenguni, shirika lisilo la kifaida ambalo linamudu rasilmali za mtandao kwa manufaa ya umma. Inajulikana kwa wadhifa wake kama mwendeshaji wa kiufundi wa mfumo wa majina mtandaoni (Domain Name System).

Makao yake makuu ni Los Angeles, California, Marekani. ICANN ina vitovu Istanbul, Los Angeles, na Singapore. Pia ina afisi shirikishi Beijing, Brussels, Montevideo, Washington, na Nairobi.

Malengo[edit | edit source]

Kusimamia, kwenye kiwango kikuu, mfumo wa kipekee ulimwenguni wa vitambulisho mtandaoni, na haswa kuhakikisha udhabiti na usalama wa utendajikazi wa mfumo wa kipekee ulimwenguni wa vitambulisho mtandaoni.

Haswa, ICANN:

  1. Inasimamia ugavi na utekelezaji wa vitengo vitatu vya utambulisho kwa ajili ya mtandao, anbavyo ni:
    • Mfumo wa Majina (Domain names); ambao unaunda mfumo unaoitwa DNS)
    • Itifaki za anwani na mfumo huru wa nambari (Internet protocols)
    • Kiunganishi itifaki na nambari zinazotofautiana
  2. Inazingatia uendeshaji na ukuzaji wa mfumo wa sava za nambari {DNS root name server system}
  3. Inazingatia uundaji wa sera kwa njia mwafaka na inayowiana na majukumu ya kiufundi

Utawala[edit | edit source]

Bodi ya viongozi wakuu: 16 wanaopiga kura na washirika wakilishi 5.

ICANN iliundwa mnamo 1998 chini ya sheria za jimbo la California. Uendeshaji wa majukumu yake ulianza chini ya mkataba wa makubaliano na idara ya kibiashara ya Marekani.

IANA Stewardship Transition[edit | edit source]

Kipindi cha Mpwito cha IANA[edit | edit source]

Mnamo tarehe 14 Machi 2014, Wizara ya biashara ya Marekani kupitia idara ya kitaifa inayosimamia mawasiliano na habari NTIA ilitangaza nia yake ya kukabidhi mamlaka yake ya kuendesha majukumu ya IANA kwa jamii ya washika dau ulimwenguni. Mapendekezo haya yalinakiliwa kuwa matukio muhimu sana kwenye historia ya mtandao {Internet}.

Kipindi hiki cha mpwito kilikadiriwa kukamilika kufikia tarehe 30 Septemba 2015. Hata hivyo, baada ya kuzingatia swala la muda, ukusanyaji wa maoni kutoka kwa umma, upigaji msasa wa serikali ya Marekani, na utimizaji wa pendekezo hili, jamii ya mtandao ilibashiri kuwa ingechukua hadi kipindi cha mwaka mmoja kwa swala hili kukamilishwa.

Kufuatia maelekezo kutoka NTIA, ICANN iliunda kitengo cha IANA Stewardship Transition Coordination Group, ambacho kilishirikisha watu 30 kutoka makundi 13 tofauti. Kila kikundi kiliwajibika kuunda kikundi tendakazi kubuni mapendekezo yao binfasi.

Kwa upande wake, jamii ya Numbering Resource Community ilijumuisha Number Resource Organisation –NRO, kitengo cha Address Supporting Organisation -(ASO). Mashirika ya matano ya kimaeneo RIRs yanayosimamia maswala ya usajili wa rasilmali za mtandao yaliunda kundi la pamoja Consolidated RIR IANA Stewardship Proposal Team- (CRISP Team) kushughulikia pendekezo lao.

Kwa upande mwingine, jamii ya Protocol Parameters ilijumuisha Internet Architecture Board IAB na Internet Engineering Task Force IETF na kuunda kitengo cha IANAPLAN Working Group. Vivyo hivyo, jamii ya Domain Names iliunda vikundi viwili: Cross Working Group CWG) Stewardship, na Community Cross Working Group CCWG Accountability.

Kwenye kongamano la ICANN 55 liloandaliwa Marrakech-Morocco, kundi la utekelezaji mapendekezo IANA Transition Coordination Group -ICG liliwasilisha mapendekezo ya mwisho ya ukabidhi wa majukumu ya IANA IANA functions.
Mapendekezo haya ya mwisho yalipokelewa na bodi ya ICANN mnamo tarehe 10 machi 2016, na baadaye kukabidhiwa kwa NTIA ili kupitishwa.

Baraza la Kongres Marekani lilianza kuyapitia maoni ya mapendekezo ya IANA. Baraza hilo la Kongres lilikuwa na muda wa hadi Septemba 2016 kutoa hatma yake. Kufikia 9 Juni 2016, NTIA ilitoa taarifa ya kuonesha kuridhishwa kwake na mapendekezo ya kukabidhi mamlaka ya uendeshaji majukumu ya (IANA)kwa jamii ya washika dau ulimwenguni.

Jamii ya mtandao ilikuwa na hofu kwamba muda haungeruhusu kupitia na kupitisha mapendekezo hayo. Hata hivyo, kulikuwepo na uwezekano wa kuongeza miaka mitatu zaidi kama ilivyokubaliwa kwenye mapendekezo ya utekelezaji {implementation proposal} kufanikisha shughuli hii nzima.