Majadiliano:Main Page

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

HTML (Hypertext Mark-up Language)[edit source]

HTML (Hypertext Mark-up Language)ni msimbo au lugha inayotumika sana ketengeneza kurasa za wavuti, na kuandaa taarifa kwa ajili ya maonyesho kwenye wavuti.

Ghafi huelezea Kivinjari jinsi ya kuonyesha maneno, picha na ishara zingine kwa mtumiaji. HTML ipendekezwa rasmi na Kingamoano la Mtandao Ulimwenguni (World Wide Web Consortium - W3C). Kwa ujumla, HTML imezingatiwa na vivinjari maarufu duniani kama vile Firefox. Toleo rasmi la sasa la HTML ni HTML 4.0.

CERT (Computer Emergency Response Team) ni kundi la magwiji wa usalama wa teknohama vinavyoundwa kwenye nyanja za kitaifa, au kimashirika na malengo ya kuzuia mashambulizi ya kimtandao.

TTCL ni kifupisho cha maneno ya kiingereza TANZANIA TELECOMMUNICATION COMPANY LIMITED. TTCL ni shirika la umma ambalo hufanya kazi ndani ya nchi kwa ujumla, ambapo hutoa huduma mahususi za kimawasiliano kwa wafanyabiashara, watu binafsi na hata serikali. TTCL ilianzishwa mwaka 1994 baada ya kuvunjika kwa TPTC (Tanzania Posts and Telecommunications Corporation). Mvunjiko wa TPTC ulipelekea mgawanyiko baina ya mawasilianao ya kimtandao na yale ya huduma ya posta, banki ya posta na hivyo kupelekea kuwepo kwa mamlaka inayojitegemea ya udhibiti wa mawasiliano. Tarahe 23 mwezi wa pili, mwaka 2001, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini makubaliano ya ubinafsishaji baina yake na wawekezaji wa kimkakati. Kundi hilo la wawekezaji lilijumuisha DETECON ya Ujerumani na MSI (Mobile Systems International Cellular Investments Holdings BV) ya Nethalandi (ambayo baadae ilibadilika na kuwa Celtel International BV na Bharti Airtel Tanzania BV). Katika makubaliano, MSI ilichukua 35% ya hisa toka TTCL na hisa zilizosalia za 65% kuchukuliwa na serikali. Japo kuwa Serikali ingali katiaka mchakato wa kununua hizo hisa isizozimiliki na hivyo kupelekea TTCL KUMILIKIWA NA Serikali kwa 100%.

REFERENCE:

https://www.ttcl.co.tz/abt_missionvission.asp Accessed on 16th August 2016 at 11:56 PM