Project:Sera ya faragha

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

ICANN (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers)
Shirika lisilo la kifaida lenye makao yake makuu jiji la Los Angeles, California, Marekani lilianzishwa sptemba 18,1998.
ICANN inamudu rasilmali za mtandao kwa manufaa ya umma. ICANN inajulikana kwa wadhifa wake kama mwendeshaji wa kiufundi wa mfumo wa majina mtandaoni (Domain Name System).
http://www.icann.org/


ICANNWIKI: Ni shirika la kijamii ambalo limejitolea kusaidia ushirikiano wa jamii ya mtandao unaolenga kubuni makala ya ICANNwiki kuhusu ICANN na mijadala inayaohusiana na utawala wa mtandao. Wiki inatoa taarifa isiyoegemea upande wowote kwa wale wanaoshiriki mikutano ya ICANN, na jamii ya mtandao kwa jumla.


ICANNFELLOW: Ni mtu yeyote anayechaguliwa kwenye program ya ICANN Fellowship.


ICANNFELLOWSHIP: Ni ratiba ya ICANN inayofanyika kwenye kila kongamano la ICANN kwa malengo ya kuwawezesha vijana kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kuwa viongozi wa siku za usoni kwenye nyanja ya utawala wa mtandao. http://www.icann.org/resources/pages/fellowship-2012-02-25-en


AFRINIC (African Network Information Center) 
Ni mojawapo ya mashirika matano ya kimaeneno(RIRs) yenye kutoa rasilimali za mtandao. AFRINIC inawakilisha bara la Africa na ukanda wa bahari ya bara hindi. Shirika la AFRINIC lilianzishwa February 22, 2005 na makao yake makuu ni mji wa Ebene, Mauritius. 
Mkurugenzi mkuu wa AFRINIC ni Alan Barrett kutoka Afrika Kusini.
http://www.afrinic.net/ADR (Alternative Dispute Resolution)
Ni njia mbadala ya kisheria inayoruhusu wanaozozana haswa kwenye maswala ya mtandao, kusulihisha migogoro nje ya mahakama kupitia mashauriano na maelewano.


AFRISIG (African School of Internet Governance)
Ni mradi unaolenga kuwahudumia waandaaji na wazungumzaji wa makongamano ya utawala wa mtandao kimataifa, kimaeneo, na kitaifa kwenye eneo la AFRINIC kupitia kozi za hali ya juu zinazoshughulikia mijadala ya utawala wa mtandao.
Darasa la kwanza la AFRISIG liliandaliwa Durban, Afrika Kusini kutoka 10-12, likiwalenga washiriki 35 kutoka mataifa 15 ya Afrika
 Darasa la pili la AFRISIG liliandaliwa Mauritius kutoka 21-25 Novemba 2014, na kushirikisha washiriki 50 kutoka mataifa 20 ya Afrika
Darasa la tatu la AFRISIG liliandaliwa Addis Ababa, Uhabeshi: 1-5, Septemba 2015. #AfriSIG2015, ilhali la nneAfTLD (The Africa Top Level Domains Organization) 
afTLD ni ushirikiano wa wasajili wa majina ya ngazi ya juu mtandaoni kwa nchi zilizopo (ccTLD) barani Afrika. Lengo kuu la AfTLD ni kusaidia wasajili wa ccTLD kujadili maswala ibuka yanayoguzia uendeshaji wa ccTLD, na vile vile kutoa msimamo mmoja kuhusu changamoto za mfumo wa majina (DNS) duniani.AIS (Africa Internet Summit)
Ni kongamano linaloandaliwa kila mwaka na AFRINIC ili kuwaleta pamoja washika dau tofauti tofauti ili kujadili maswala nyeti yenye umuhimu kwa maendeleo ya mtandao barani Africa. Mwaka huu (2016), kongamano hili limefanyika jijini Gaborone, Botswana.

APC (Association for Progressive Communications)
Ni shirika na vile vile mtandao wa kimataifa wa mashirika ya kijamii wenye malengo ya kuwezesha mashirika na watu binafsi kupata huduma nafuu za mtandao kwa ajili ya maendeleo.
APC ina wanachama 50 katika mataifa 35, mengi yayo yakiwa kutoka mataifa yanayoendelea.APC ilianzishwa mnamo 1990 na inaongozwa na sheria za jimbo la California.
Afisi kuu ya uendeshaji shughuli za APC ipo Johannesburg, Afrika kusini.
http://www.apc.org/APNIC (Asia-Pacific Network Information Centre) Mojawapo wa mashirika matano ya kimaeneo (RIRs) yenye kutoa rasilmali za mtandao. APNIC inawakilisha bara Asia na eneo la bahari ya kusini 
http://www.apnic.net/


ccTLD (country code Top Level Domain)
Neno lenye nukta mbili zinazoashiria utambulisho wa nchi mtandaoni mfano .ke (Kenya), .tz (Tanzania), zinazoendeshwa na meneja wa nchi husika.
http://www.icann.org/en/resources/cctldsCERN (European Centre for Nuclear Investigtions)
Ni mradi wa kisayansi wenye makao yake Geneva, Uswisi ambao ulichangia pakubwa kwenye teknohama kupitia uvumbuzi wa WWW na mtandao kwa jumla.
http://home.web.cern.ch/CERT (Computer Emergency Response Team)
Ni vikundi vya magwiji wa usalama wa teknohama vinavyoundwa kwenye njanja za kitaifa, au kimashirika na malengo ya kuzuia mashambulizi ya kimtandao.
http://www.enisa.europa.eu/activities/certCIPIT (Centre for Intellectual Property in Information Technology)
Ni kituo kilichopo ndani ya chuo cha Strathmore, kinachojihusisha na maswala ya hakimiliki kwenye nyanja ya teknohama, na jinsi haki miliki hizi zinavyoathiri sheria na haki za kibinadamu barani Afrika.
www.cipit.org 
CJEU (Court of Justice of the European Union)
Mahakama ya haki ya umoja wa nchi za ulaya inayotatua maswala na kuhakikisha sheria zinatekelezwa kote kwenye washirika wa umoja huo.


CoE (Council of Europe)
Shirikisho la umoja wa ulaya lenye nchi 47 ambazo zinalipa swala la utawala wa mtandao kipa umbele mfano usalama mtandaoni, haki za kibinadamu mtandaoni, ulindaji wa taarifa kuhusu watu na kadhalika.
http://hub.coe.int/ 
COFEK (Consumer Federation of Kenya)
Ni muungano unaotetea haki za watumiaji bidhaa na huduma nchini Kenya.COP (Child Online Protection)
Usalama wa watoto mtandaoni kutokana na matishio yanayotakana na mtandao.


CPRSouth (Communication Policy Research South)
Ni mradi unaojenga uwezo wa kuendeleza wasomi waliopo eneo la Asia na bahari ya kusini, na Afrika kwenye njanja ya sera ya teknohama. 
CPRSouth inalenga haswa wasomi wa kiwango cha chini, na vile vile cha kati. 
CPRSouth ilizinduliwa mnamo 2006, huku kongamano lake la kwanza la sera ya teknohama likiandaliwa Januari 2007 jijini Manila, Ufilipino.
Mnamo Aprili 2010, CPRSouth ilizindua mradi wa CPRAfrika, wenye makao yake Cape Town, Afrika Kusini. Mradi huu wa CPRSouth unafadhiliwa na shirika la IDRC la Canada.
Agosti mwaka huu, kongamano la CPRSouth litafanyika kisiwani Zanzibar.


CSCG (Civil Society Coordination Group)
Muungano wa mashirika ya kijamii unaolenga kuafikia na kutoa maamuzi kwa sauti moja.

CSK (Computer Society of Kenya) Ni muungano unaowashirikisha wataalamu wa sekta ya habari, mawasiliano na teknohama nchini Kenya.CTO (Commonwealth Telecommunications Organisation) Ni shirika la jumuiya ya madola ambalo limepata kuhuduma kwa muda mrefu sana ulimwenguni.
Linajihusisha na maswala ya maendeleo kwenye nyanja ya matumizi ya teknohama kwa ajili ya kujiendeleza kijamii na kiuchumi.
Lilianzishwa mnamo mwaka wa 1901, japo limekuwepo katika hali yake ya sasa ya ushirikano baina ya mataifa tokea 1967. Wanachama wake ni kutoka nchi zilizoendelea sana, zinazoendelea, zilizo na maendeleo duni. 
Makao yake makuu ni London, uingereza.


DNSAFRICA Magazine
Ni jarida linalochapishwa na kampuni ya DNS Africa Communications.
Nakala za jarida hili huguzia mijadala inayohusu ICANN na mfumo wa majina (DNS), barani Afrika na ulimwenguni. DNSSEC (Domain Name System Security)
Teknolojia ya kiusalama kwenye DNS.
http://www.icann.org/en/about/learning/factsheets/dnssec-qaa-09oct08-en.html


DoC (Department of Commerce)
Idara ya kiuchumi na biashara ya Marekani. Idara hii ina umuhimu mkubwa kwenye utawala wa mtandao kwa sababu ndio iliyotwikwaa uwezo na mamlaka ya kusimamia shughuli za ICANN.
http://www.commerce.gov/


DoD (Department of Defense)
Idara ya ulinzi wa Marekani. Idara hii ilijihusisha na na mradi wa DARPANET na kipindi cha mwanzo wa mtandao.
http://www.defense.gov/


dotAfrica (.Africa)
.Africa ni jina la ngazi ya juu kwenye mtandao lililoidhinishwa na ICANN kwa ajili ya bara la Afrika na jamii zinazoegemea Afrika. .Africa gTLD itahudumu kama jina la eneo la Afrika na eneo la bahari ya bara hindi, na vilevile kwa wale ambao wapo maeneo tofauti nje ya bara.
www.africainonespace.org


EAIGF (East Africa IGF)
Ni kongamano la utawala wa mtandao la eneo ya Afrika mashariki linalofanyika kila mwaka kujadili maswala ibuka yenye umuhimu kwenye mtandao na matumizi yake mfano usalama, ujasusi n.kEC (European Commission)
Tume inayowakilisha bara ulaya. Tume hii inajumuisha wahudumu 28 wanaopendekeza na kuhakikisha sheria zinafuatwa na wanachama.
http://ec.europa.eu/ 

E-government (Electronic government)
Inaashiria matumizi ya vifaa vya habari, mawasiliano, na teknohama kuboresha shughuli za utoaji huduma kwa mashirika ya umma.


E-learning (Electronic learning)
Masomo yanaoendeshwa ki-elektroniki kupitia mtandao.


EuroDIG (European Dialogue on Internet Governance)
Kongamano la bara ulaya linalojadili maswala ya utawala wa mtandao. EURODIG ilianzishwa 2008 na mashirika tofauti, wawakilishi wa serikali na magwiji ili kuendeleza mjadala na ushirikiano na jamii ya mtandao kuhusu sera za umma kwa ajili ya mtandao. EURODIG huandaliwa kila mwaka kwenye mji mkuu tofauti EuroDIG inafadhiliwa na vikundi vya wafadhili wa mashirika husika, mfano kamati ya Ulaya (Council of Europe –CoE), Umoja wa Ulaya (EU), European Regional At-Large Organization (EURALO), the European Broadcasting Union (EBU), ICANN, ISOC, the Federal Office of Communications of Switzerland (OFCOM) and the Ré- seaux IP Européens Network Coordination Centre (RIPE NCC). 

http://www.eurodig.org/


Europol (European Police)
Kitengo cha usalama kinachisaidia mataifa wanachama wa EU kupigana na uhalifu na ugaidi.
https://www.europol.eu/


EUROSSIG (The European Summer School on Internet Governance) Ni shule inayolenga kuwahudumia waandaaji na wazungumzaji wa makongamano ya utawala wa mtandao kimataifa, kimaeneo, na kitaifa kwenye eneo la bara ulaya kupitia kozi za hali ya juu zinazoshughulikia mijadala ya utawala wa mtandao. Tofauti na APSIG na AFRISIG, EUROSSIG inalenga washiriki kutoka mataifa mbali mbali kutoka kote ulimwenguni, huku mataifa yanaoendelea yakipewa kipa umbele.
Masomo ya EUROSIG yanadumu juma nzima na yanafanyika kila mwaka (Julai) jumla ya masaa 48. Kozi hizi zinaguzia mijadala ya utawala wa mtandao kama vile siasa, sheria, uchumi, tamaduni za jamii, ufundi wa teknohama.


IANA (Internet Assigned Names and Authority)
Ni tawi dogo la ICANN linalosambaza rasilmali muhimu za mtandao (IP). IANA inawajibika kugawa rasilmali za IP kwa mashirika matano ya mtandao kimaeneo (RIRs)
http://www.ntia.doc.gov/page/iana-functions-purchase-order


ICANN Learn 
Ni uga huria na wa wazi unaowezesha jamii ya mtandao duniani kufanya kozi zinazohusiana na mijadala ya ICANN na utawala wa mtandao
http://learn.icann.org/


ICC (International Chamber of Commerce)
Shirika la kushughulikia maswala ya biashara duniani lenye makao yake Paris, Ufaransa.
http://www.iccwbo.org/


ICG (IANA Stewardship Transition Coordination Group)
Kundi la kujadili na kuafikia mijadala inayohusu NTIA/ICANN/ na kipindi cha mpwito cha IANA (IANA Transition).ICT (Information and Communication Technology)
Neno linaloelezea matumizi yote ya teknohama. Mbinu na matumizi yake ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi, kulingana na mtazamo wa ITU.
http://en.wikipedia.org/wiki/Information_and_communications_technology 
ICTA (ICT Authority)
Ni tume ya serikali ya Kenya iliyoundwa chini ya idara ya habari, mawasiliano na teknohama ili kusimamia shughuli zinazoambatana na sekta hii. IDN (Internationalised Domain Name)
 Majina ya mtandaoni yanayoruhusu nukta zisizo kwenye alfabeti ya kilatini mfano kiarabu, kirusi, kichina.
http://en.wikipedia.org/wiki/Internationalized_domain_nameIEEE (Institute of Electrical and Electronics Engineers)
Shirikisho linaloazimia kuendeleza teknohama na ubunifu.
http://www.ieee.org/about/ieee_history.html


IETF (Internet Engineering Task Force)
Shirika la kiufundi la mtandao lenye uhusiano na ISOC.
http://www.ietf.org/


SOC (Internet Society)
Ni shirika la kimataifa, lisilo la kifaida ambalo lilizinduliwa mwaka 1992 na Vint Cerf – mvumbuzi wa TCP/IP, na lengo la kutoa mwongozo kwenye maswala yanayohusiana na (standards) mtandao, elimu, matumizi, na sera.
Maono yake ni kuendeleza uwazi, mabadiliko na matumizi ya mtandao kwa manufaa ya watu wote ulimwenguni. 

ISOC inajumuisha vitengo kama vile Internet Engineering Task Force (IETF), Internet Architecture Board (IAB), Internet Engineering Steering Group (IESG), na Internet Research Task Force (IRTF). Makao makuu ya ISOC yapo Reston, Virginia, Marekani (karibu na Washington, D.C.), afisi zake zipo Geneva, Uswisi. ISOC ina uanachama wa zaidi ya mashirika 140, na wanachama wa 80,000 wa kibinafsi.
Wanachama pia huunda makundi (chapters)kulingana na kanda walizomo au uraibu wao. Kuna makundi (chapters) zaidi ya 110 ulimwenguni.
http://www.internetsociety.orgISP (Internet Service Provider)
Shirikia (haswa la kibiashara) linalotoa huduma za kuunganisha watu kwenye mtandao.


TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) Ni asisi ya serikali inayodhibiti shughuli zote zinazohusiana na mawasiliano nchini Tanzania. Asisi hii iliundwa mnamo 2003 ili kusimamia mawasiliano ya ki-elektroniki, huduma za Posta, na usimamizi wa wigo wa kitaifa wa urushaji mawimbi. Asisi hii ilianza majukumu yake rasmi mnamo tarehe 1 Novemba 2003, na kuchukua pahala pa iliyokuwa tume ya mawasiliano Tanzania(TTC) na tume ya Utangazaji (TBC) Makao makuu ya asisi hii ni jijini Dar es Salaam.


TzNIC (Tanzania Network Information Center) Ni shirika Iisilo la kifaida lililobuniwa na tume ya mawasiliano ya Tanzania (TCRA) ili kuendesha oparesheni na usajili wa jina la ngazi ya juu la nchi mtandaoni (.tz). TzNIC iliundwa mnamo 16 Novemba, 2006. Kufikia sasa, TzNIC ina sajili za .tz karibia 12,000. Hivi majuzi, tume ya TCRA ilitoa makataa kwa kampuni zote nchini Tanzania kusajili na .tz


.TZ (DOTTz)
Ni jina la ngazi ya juu mtandaoni kwa nchi ya Tanzania lililozinduliwa mnamo 1995.
Msajili wa .tz ni tzNIC, ilhali mfadhili mkuu wake ni chuo kikuu ya Dar es Salaam.


NIC (Network Information Centre)
Inaashiria mashirika matano ya kimaeneo (RIRs) yanayojihusisha na ugavi wa rasilmali muhimu za mtandao (IP). Mashirika hayo ni AFRINIC, APNIC, ARIN, LACNIC, na RIPE NCC.


IP (Internet Protocol)
IP ni nambari za kipekee zinazosaidia kwenye kutambua kila kifaa kilichounganishwa kwa mtandao mfano tarakilishi, kipakatalishi, tabiti, kamera, simu, na printa.
Mfumo wa ugawaji wa nambari za IP umepangwa kwa ngazi ya aina yake: Juu kuna IANA – tawi dogo la ICANN, ambalo linagawa rasilmali za IP kwa mashirika matano ya mtandao kimaeneo (RIRs).
RIR zinagawa nambari hizi za IP kwa mashirika ambayo hutenga rasilimali hizi kwa mashirika madogo (LIRs), kampuni, na watu binafsi waliopo chini zaidi ya mpangilio wa ngazi. IPR (Intellectual Property Rights)
Haki miliki kwa mwenye kubuni au kuzindua kitu.


dotAfrica (.Africa)
.Africa ni jina la ngazi ya juu kwenye mtandao lililoidhinishwa na ICANN kwa ajili ya bara la Afrika na jamii zinazoegemea Afrika. .Africa gTLD itahudumu kama jina la eneo la Afrika na eneo la bahari ya bara hindi, na vilevile kwa wale ambao wapo maeneo tofauti nje ya bara.
www.africainonespace.org


HTML (Hypertext Mark-up Language)
Msimbo au lugha inayotumika sana ketendeneza kurasa za wavuti, na kuandaa taarifa kwa ajili ya maonyesho kwenye wavuti.
http://en.wikipedia.org/wiki/HTML


RTC (Real Time Chat)
Ni uwezo wa kupokea jumbe kwenye mtandao kwa wakati mwafaka, pindi zinapotumwa.
 .RW (DOTRW)
.rw ni ni jila la usajili la ngazi ya juu mtandaoni kwa nchi ya Rwanda
.rw ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1996.


RFC (Request for Comments)
Inatumiwa kuashiria machapisho ya IETF. Machapisho haya yalizinduliwa mwaka wa 1969 na Steve Crocker, mwanabodi wa sasa wa ICANN, kunakili matukio ya ARPANET. Siku hizi yanatumiwa kunakili mapendekezo ya mwelekeo wa mtandao, na itifaki za mawasiliano.RIPE NCC (Réseaux IP Européens Network) Ni mojawapo wa mashirika matano ya kimaeneo (RIRs), linalosimamia ugavi wa rasilmali muhimu za mtandao (IP) eneo la bara ulaya.


RIR (Regional Internet Registry)
Mashirika yasiyo ya kifaida ambayo yanasimamia na kuendesha shughuli za ugavi wa rasilmali za mtandao (IP). Kuna mashirika 5: AFRINIC, APNIC, ARIN, LACNIC, na RIPE NCC. Mashirika haya hufanya kazi kwenye miradi kwa pamoja.

RSSAC (Root Server System Advisory Committee)


RSSAC inawajibika na utoaji ushauri kwa jamii ya ICANN, na wanabodi kuhusu maswala yanayoguzia oparesheni, usimamizi, usalama,na hadhi ya mfumo wa Root Server (Root Server System), kama ilivyo kwenye mwongozo wa sheria ndogo za ICANN.
ToS (Terms of Service)
Makubaliano ya huduma, au sheria na vigezo ambavyo anayepania kutumia huduma fulani mtandaoni anahitaji kusoma, na kukubali kama sehemu ya mkataba wa makubaliano kabla ya kutumia huduma hiyo.TRIPS (Trade Related Aspects of Intellectual Property Rights) http://www.wto.org/english/thewto_e/whatis_e/tif_e/agrm7_e.htm 
Ni sheria zinazohusiana na haki miliki zilizotokana na mkataba wa WTO.TTIP (Transatlantic Trade and Investment Partnership)
Ni mkataba huria wa biashara na uwekezaji baina ya Marekani na umoja wa Ulaya (EU). Mkataba huu umeweza kufutiliwa mbali na rais Donald Trump pindi tu alipoingia madarakani.WAIGF (West Africa Internet Governance Forum)
Ni kongamano la utawala wa mtandao la eneo ya Afrika ya magharibi linalofanyika kila mwaka kujadili maswala ibuka yenye umuhimu kwenye mtandao na matumizi yake mfano usalama, ujasusi n.kW3C (World Wide Web Consortium)
Jamii ya kimataifa yenye wanachama na wafanyakazi wanaohuduma kuunda sera zenye kulenga ubora kwenye mtandao.Jamii hii inaongozwa na mvumbuzi wa WWW Tim Berners-lee na mkurugenzi mkuu Jeffrey Jaffe.
Ruwaza ya Wc3 ni kuongoza mtandao kwa uwezo wake kamili.
WCIT (World Conference on International Telecommunications) http://www.itu.int/en/wcit-12/Pages/default.aspx 

WGIG (Working Group on Internet Governance)
Tume iliyobuniwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya hatua kuhusu utawala wa mtandao (Internet Governance).

WHOIS 
Hifadhi iliyo wazi kwa umma inayoonyesha taarifa za mashirika, na vile vile watu binafsi. Taarifa za hifadhi hii zinahusiana na usajili wa rasilimali za mtandao kama vile nambari za kipekee (IP), na majina (Domain Names)

WIPO (World Intellectual Property Organisation)
Kitengo cha umoja wa mataifa (UN) ambacho kinahusika haswa na maswala ya haki miliki kama njia moja ya kukuza ubunifu. WIPO iliundwa 1967 “kuwezesha ubunifu, na kuendeleza ulindwaji wa haki miliki kote duniani.


WIPO ina mataifa wanachama 188, nainasimamia mikataba 26 ya kimataifa. Makao yake makuu ni Genevea, Uswisi.
Mkurugenzi mkuu wa sasa wa WIPO ni Francis Gurry, ambaye alitwaa uongozi Octoba1, 2008. Mataifa yasiyo wanachama wa WIPO ni visiwa vya Marshall, Mkusanyiko wa visiwa vya Micronesia, Nauru, Palau, Visiwa vya Solomon, Sudan Kusini, Timor-Mashariki, Palestina na yana hadhi ya utazamaji tu

WITSA (World Information Technology And Services Alliance)
Ni muungano ulioanzishwa kwa ajili ya kuwaunganisha wanachama waliopo kwenye sekta ya teknohama katika mataifa mbali mbali.

WSIS (World Summit on Information Society)
Kongamano lililofanyika kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilifanyika Geneva, Uswisi tarehe 10 hadi 12 Disemba 2003; awamu ya pili ilifanyika Tunis, Tunisia kutoka tarehe 16 hadi 18 Novemba 2005.