TzNOG DODOMA

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

tzNOG ni umoja au kikundi kinachotoa mafunzo kwa wataalam wa Tehama kwa gharama nafuu hapa hapa nchini. Jitihada za kikundi hiki ni kuongeza ushiriki wa wataalam wa Tanzania kwani mafunzo kama haya (afnog) yafanyikapo nje ya nchi ghrama zake huwa ni kubwa sana na wengi wao kushindwa kushiriki.

Kwa sasa tzNOG ina mafunzo katika makundi (tracks) 4 – Network Management & Monitoring (NMM), Scalable Internet Services (SIS), Systems and Network Security (SNS) and Routing & Switching (R&S).

Lengo la mafunzo haya ni kufanyika kila mkoa na mpaka sasa mafunzo haya yameendeshwa katika mikoa 5 – Arusha (2013), Mwanza (2014), Zanzibar (2015), Dar es Salaam (2016) na Dodoma (2017). Masomo yaliyofundishwa katika mikoa hiyo ni Arusha (NMM & SNS), Mwanza (SNS na R&S), Zanzibar (NMM, R&S and SNS) na Dar es Salaam (R&S). Sababu za kubadilisha masomo ni kuongeza mvuto kwa washiriki na pia kulenga kukidhi mahitaji wa washiriki.


TzNOG5 Dodoma Katika mafunzo haya masomo 2 yamechaguliwa na ni SIS na SNS. Sababu kuu ni kutokana na suala la usalama mtandaoni ambalo limepewa kipau mbele sana na pia suala la kuendesha mail na web servers kwa umakini.

Kwa mara ya kwanza kabisa wakufunzi wa masomo haya ni watanzania pekee. Katika miaka ya nyuma tumekuwa pia na wakufunzi toka nje ya nchi (Kenya, Uganda, Marekani, Afrika kusini, Uingereza, Denmark na New zealand).

Tokana na ada ndogo ya washiriki, kamati ya maandalizi inafanikisha mafunzo haya kwa ufadhili wa wadau mbali mbali. Kwa mwaka huu ufadhili umetoka TISPA, TCRA, TTCL, AfriNIC, tzNIC na ISOC

Mpaka sasa tzNOG imefanikiwa kutoa mafunzo kwa washiriki 278 ukijumisha na washiriki 56 walioshiriki tzNOG5.

Changamoto kubwa ya uandaaji wa mafunzo haya nu upatikanaji wa ufadhili kwani ni makampuni machache sana ambayo yanaelewa jitihada za tzNOG na umuhimu wa mafunzo kwa wafanyakazi wake.


imetolewa na Zuhura Msisi[edit | edit source]