Usalama wa mifumo na mitandao

From Swahili ICANNWiki
Jump to: navigation, search

usalama wa mifumo na mtandao kwa siku zijazo itakua ngumu sana kutofautisha maisha ya mtu na technilojia, maisha ya watu yatakua yameingiliana sana kiasi kwamba mtu anaweza kusema hawezi ishi bila kutegemea kipande fulani cha technolojia. lakini swali kubwa linabakia ni kwamba, unajua jinsi ya kujilinda tukiwa huko kwenye mifumo na mtandaoni, hapa ndipo tunapokutana na somo la usalama wa mifumo na mitandao (system and network security). kiukweli mitandao imeleta njia mpya za wizi na udanganyifu katika jamii lakini pia imeboresha njia za uhalifu na udanganyifu wa zamani na kuufanya wa kisasa hivyo kuongeza uhalifu kwa ujumla. kwa sasa ni mara chache sana kusikia mtu amekabwa kichochoroni lakini tumeanza kuzoea kusikia wizi wa taarifa za watu kwenye mitandao, wizi wa utambulisho wa watu na mambo mengine mengi yanayoendana na hivyo na imekua ni mambo ya kushtusha sana jamii tofauti na mashambulizi ya kimwili yanayotokea. kiukweli dunia imebadilika sana na kwa sasa tunatakiwa tujifunze zaidi jinsi gani ya kujilinda ili madhara haya yasije kujitokeza kwako.


imetolewa na Zuhura Msisi